• Wed. Sep 18th, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

Bodaboda eneo la Soweto waandamana dhidi ya Babu Owino,Nicholas Okumu

Jun 16, 2021
441 300

Waendeshaji bodaboda katika eneo la Soweto eneo la Kayole waliandamana hiyo jana kulalamikia barabara mbovu inayounganisha eneo la Soweto na Mtaa wa Embakasi.


Wanabodaboda hao walisema kuwa juhudi zao za kuwataka viongozi kuwaundia barabara hiyo hazijakuwa zikizaa matunda na ndio sababu wakaamua kuandamana. Wanasema kuwa, wamekuwa wakitumia pesa nyingi katika kuzikarabati bodaboda zao na wanapata hasara kubwa sana.


Barabara hiyo ambayo haijawekwa lami na imejaa mashimo pia. Kwa masaa kadhaaa walifunga barabara waliandamana na kuchoma magurudumu wakitaka barabara hiyo kuundwa.

Lawama hizo hizo wamemwekelezea mbunge wa eneo hilo Paul Ongili anaye julikana kwa wengi kama Babu Owino. Wanasema amekuwa akiwapuuza kila wamnapotoa lalama zao kuhusu barabara hiyo.


“Babu alitudanganya atatengeneza barabara. Tumechoka na vumbi iliyojaa katika barabara hii. Unaona hata polisi ndiohao waanakuja kutusumbua. Wakati tunataka usaidizi mwakilishi wodi Nicholas Okumu hata hatumjui. Akija hapa akiona vumbi hii anafunga vioo vya gari. Tunawaulia tuliwachagua wakae kwa ofisi ama watusaidie? Wananchi Tunaumia, tunakaa ni kama tumepakwa rangi,tunataka haki yetu,” alisema Griffin Mzee mkaaji wa Soweto.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *