Mzee mwenye umri wa miaka themanini katika kata ya Chevaywa, Matete Kaunti ya Kakamega ametiwa mbaroni na maafisa wa polisi baada ya kumnajisi mtoto wa miaka minne, kutoka kata ndogo ya Marakusi.
Kulingana na Afisa wa watoto, Bwana.Jackson Murunga, mtoto huyu alikuwa amezoea kukaa na Babu huyo nyakati za mchana kabla yake kumgeukia na kumtendea unyama huo na kumjeruhi vibaya.
Inadaiwa mzee huyo alimpoteza mkewe Zaidi ya miaka kumi iliyopita na muda ambao amekuwa akikaa na mtoto huyo ulifanya Wazazi wake kuwa na uhakika alikuwa salama.
Akidhibitisha Tukio hilo, Bwana Murunga alisema kuwa baada ya kutekeleza unyama huo, mzee huyo alienda mafichoni alikotafutwa na maafisa wa kituo cha matete na kutiwa mbaroni baadaye.
Uchunguzi umebainisha kuwa mtoto huyo alinajisiwa na anapokea matibabu hospitalini.