Askari wa Gereza la Kangeta eneo la Igembe aliyetambuliwa Kama Edwin Mouse anatafutwa baada yake kuonekana akiwa na bunduki aina ya G3 akiwa ameificha kwenye gunia.
Inasemekana Kuwa askari jela huyo aliyeonekana katika soko la Kangeta na mwenzake Carolyn Wambui akataarifuwa Kuwa alikuwa anaelekea sehemu za Thika kutekeleza mauaji ya mkewe ambaye alichukuwa hela zake karibia shilingi Elfu mia Tisa alizokuwa amechukuwa Kama mkopo.
Bunduki hiyo aliyokuwa nayo inadaiwa Kuwa na risasi 20.
Omuse alionekana na ‘Sajenti’ Benjamin Ndunda katika soko la Kangeta na hapo akamtaarifu Carolyn ambaye ni askari jela pia katika Gereza la Kangeta.
Uchunguzi una endelezwa ili kumpata askari huyo kabla ya kutekeleza mauaji.