Wahudumu wa matatu sasa wamepata afueni hii baada ya serikali kuafikiana kubeba abiria kwenye viti vyote kuanzia Jumatatu wiki ijayo.
Katika mkutano uliofanywa pamoja kati ya wahudumu wa matatu na waziri msaidizi Chris Obure wamekubaliana kuhusu hilo lakini wametakiwa kufata kanuni za Covid 19 kikamilifu.
Mwenye kiti wa chama cha wenye matatu nchini MOA Simon Kimutai amepongeza hatua hiyo wakisema kuwa ni hatua kubwa kusimamisha biashara katika sekta ya uchukuzi hata tukipambana na Covid 19 nchini.
‘‘Ni kweli tumefanya mkutano leo na kwamba tumekubaliana na serikali kuwa kuanzia Juma tatu tunabeba abiria katika viti vyote na ni kweli tumeumia muda mrefu, lakini sasa hatua hii itafanya sekta hii kuinuka tena.’’Kimutai alisema.
Kimutai aidha amewataka wahudumu wa Matatu kuhakikisha kuwa wamefwata kanuni zote ikiwemo abiria kuvaa barakao,na kusanitize kabla ya kuingia kwenye matatu.
‘‘Tunasihi wahudumu wetu kuhakikisha kuwa abiria anavaa barakao anapoingia kwa gari,anasanitize na pia lazima wafungue madirisha kuweke hewa safi kwenye gari.’’ Aliongeza.
Kumbuka kuwa kampuni kama vile Modern Coast zilisitisha huduma zao mpaka pale serikali ya Kenya itakapokubali kubebwa kwa abiria asilimia mia moja.