• Fri. Apr 19th, 2024

Afisi ya Gavana Francis Kimemia Yavamiwa

May 20, 2021
445 300

Maafisa wa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi [EACC] asuhi ya leo wamevamia afisi kuu za Gvana wa Nyandarua katika eneo la Olkalau kutokana na Madai ya ufujaji wa Shilingi Milioni Hamsini na tano.

Maafisa hao wamechukua stakabadhi za Zabuni zinazohusiana na chapa ya Kunti ya Kampuni inayokisiwa kuwa ya mwanawe Gavana wa Kaunti hiyo, Francis Kimemia.

Kiongozi wa Tume ya Kupambana na ufisadi katika eneo la Kati Bwana Charles Rusugu, amesema kuwa walikuwa wamelenga afisi ya Gavana Kimemia na ile ya Fedha.

“Tumechukua stakabadhi kutoka kwa karani wa gavana na Afisi ya Fedha ili kukamilisha uchunguzi kutokana na madai ya zabuni iliyotolewa mwaka 2019,” Alisema Rusugu.

Aidha, alisema kuwa uchunguzi utafanywa katika afisi nyingine pia japo, ofisi hizi mbili ndizo zinazolengwa Zaidi. Ameongeza pia, hakuna aliyekamatwa lakini iwapo yeyote atafeli kushirikiana nao basi atakamatwa mara moja.

“yeyote atakaye kata kushirikiana nasi ili tukamilishe uchunguzi basi tutamkamata,” aliongeza Rusugu.

Mwaka 2019, Ndegwa Wahome aliyekuwa Spika wa kaunti ya Nyandarua alisema kuwa baadhi ya maafisa wa kaunti ya Nyandarua walifanya mkutano na kufuja hela kwa akaunti zao binafsi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *